Back to top

Makamu wa Rais atahadharisha Rushwa kuelekea Uchaguzi mkuu.

08 August 2020
Share

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amezindua Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma huku akiwataka wanasiasa na wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili kupata viongozi bora na waadilifu watakaolitumikia taifa.

Akizindua majengo hayo Makamu wa Rais Mama Samia akatumia jukwaa hilo kuwatahadharisha wanasiasa na wananchi dhidi ya vitendo vya rushwa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amemueleza Makamu wa Rais kuhusu matokeo ya tume iliyoundwa ili kuchunguza thamani ya fedha katika ujenzi wa ofisi hizo na hatua zilizochukuliwa.

Kwa upandde wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika licha ya kupongeza mafanikio yaliyofikiwa na TAKUKURU amewataka kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.