Back to top

Makosa ya mtandaoni yapungua kwa kwa asilimia 48.9.

21 May 2018
Share

Tangu kuanza kwa matumizi ya sheria ya makosa ya mtandao namba 13 ya mwaka 2015 imesaidia kupungua kwa makosa ya mtandao kwa asilimia 48.9 kati ya Januari hadi Disemba 2017 na upatikanaji wa haki pale mtu anapotenda kosa tofauti na awali.

Naibu Waziri wa wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ELIAS KWANDIKWA Amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi inaonesha kupungua kwa makosa ya mtandao hivyo uwepo wa sheria hiyo umewezesha kuimarisha matumizi salama ya mitandao.

Naibu Waziri KWANDIKWA amesema  kwa sasa serikali haina mpango wa kupeleka marekebisho ya sheria hiyo Bungeni hadi hapo kutakapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo.

KWANDIKWA amewataka wananchi kutumia fursa chanya zitokanazo na matumizi sahihi ya mitandao kuliko kutumia mitandao hiyo kuvunja sheria za nchi na maadili pamoja na tamaduni za Kitanzania.