Back to top

Makosa ya udanganyifu yabainika magari ya abiria Mwanza na Shinyanga

15 December 2018
Share

Askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga wamefanya ukaguzi wa pamoja wa magari ya abiria na mizigo katika barabara kuu ya Mwanza – Shinyanga na kubaini idadi kubwa ya magari yanye makosa yakiwemo ya udanganyifu wa madereva.

Wakizungumza kwa wakati tofauti wakuu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mukadam Mukadam wa mkoa wa Mwanza na Anthony Gwandu wa mkoa wa Shinyanga wamesema katika ukaguzi huo wamebaini kuwa bado madereva wengi hawatii sheria bila shuruti  na suala la mabasi ya abiria kuwa na madereva wawili halijazingatiwa ambapo baadhi ya mabasi yamekamatwa na kuzuiliwa kuendelea na safari.