Back to top

Makundi makubwa ya watu waingia nchini kupitia mpaka wa Namanga

19 March 2020
Share

Idadi  ya  watu  wanaoingia  nchini  kupitia  mpaka  wa  Namanga  imeongezeka  jambo linalosababisha  msongamano  mkubwa  na pia  mahitaji  ya vifaa  vya  uchunguzi  na  upimaji wa  virusi vya  Corona. 

Watendaji  wa  kituo  hicho   wamemweleza  waziri  wa  afya  Mhe.Ummy  Mwalimu  aliyetembelea  kituo  hicho  kuwa  kwa sasa  watu  kati  ya  300  hadi  500  wanapita  katika  kituo  hicho  kwa siku.
Akizungumzia  changamoto  hiyo   waziri Mhe.Ummy  Mwalimu  pamoja  na  kuahidi  kufanyia kazi  changamoto  hiyo  amewaomba wananchi  kutoa  ushirikiano   hasa  wa  kutoa  taarifa  za  watu  wanaoingia  kupitia  njia  za  panya.

Tatizo  la  mahitaji  ya vifaa  vinavyolenga  kudhibiti  maambukizi ya virusi  vya Corona  pia  imeelezwa  na    mkuu  wa  mkoa  wa Arusha  Mrisho  Gambo ambaye  amemuomba  waziri  Ummy  kuangalia  uwezekano  wa  kuweka  mashine  ya  kubaini  virusi  hivyo  katika  jiji  la  Arusha. 

Kwa  sasa watu  sampuil  za  watu  wanaohofiwa  kuwa  na maambukizi virusi  vya Corona   hulazimika  kusafirishwa hadi  jijini  Dar es Salam ambako  ndiko  iliko  maabara  yenye  uwezo  wa  kupima  virusi  hivyo.