Back to top

Makundi ya vijana wajulikanao kama PanyaRoad yaibuka Kahama.

29 April 2021
Share

Wakazi wa mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga manispaa ya Kahama Shinyanga wamelalamikia kuibuka kwa wimbi la vibaka na makundi ya vijana wajulikanao kama PanyaRoad ambao wamekuwa wakivunja nyumba na kupora mali za watu nyakati za usiku hali ambayo imezua taharuki kwa wakazi wa wilaya hiyo.
.
Malalamiko hayo yameibuka katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo ya wilaya ya Kahama.
.
Baada ya kusikiliza kero hizo Kamanda Magiligimba akawataka wananchi kutoa taarifa za wahalifu hao kwa jeshi la polisi ili waweze kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
.
Aidha Kamanda  Magiligimba amewataka wazazi wenye Watoto ambao ni wahalifu wasiwakingie kifua bali wawakemee kwa sababu uhalifu huo unatokea kutokana na wazazi kujisahau katika malezi.