Back to top

Mama Mercy Anna Mengi azikwa Machame mkoani Kilimanjaro.

10 November 2018
Share

Mwanzilishi mwenza wa makampuni ya IPP Mama Mercy Anna Mengi amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Wari, Machame  mkoani Kilimanjaro.

Mama Mama Mercy Anna Mengi alifariki Oktoba 31, mwaka huu katika hospitali ya Madicinic Morningside, Johanneburg  Afrika ya Kusini alikkkuwa akitibiwa.

Katika mahubiri yake wakati wa ibada mazishi, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT Askofu Dakta  Frederick Shoo amewataka wanadamu waishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu, ili awape aliyowaandalia baada ya maisha yao ya hapa duniani.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliotoa heshima zao za mwisho wa kwa Mama Mama Mercy Anna Mengi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT mjini Moshi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mawaziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela na Edward Lowassa, viongozi wa vyama vya siasa, wawakilishi wa taasisi mbalimbali, wakuu kadhaa wa wilaya, ndugu, marafiki na majirani.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe.