Back to top

Maofisa wa maji wafukuzwa na mbwa wasisome dira majumbani.

09 April 2019
Share

Mwezi mmoja tangu Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Mbeya kuanza kutumia viwango vipya vya bili za maji, baadhi ya wananchi wameanza kuachia mbwa na kuwatimua majumbani mwao maofisa wa mamlaka hiyo ili wasisome dira na kuandaa ankara za malipo ya maji.

Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Mbeya, Venance Hawela amesema mamlaka hiyo kuanzia mwezi Machi mwaka huu imeanza kuwatoza wateja wake viwango vipya vya ankara za maji ambavyo vimeongezeka ikilinganishwa na viwango vya zamani, jambo ambalo anadai limeibua changamoto kwa baadhi ya wananchi kutumia mbwa kuwatimua maofisa wa mamlaka hiyo wanokwenda kusoma mita majumbani.

Mwakilishi wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za maji Ewura, mkoa wa Mbeya, Magreth Tenga amewataka wananchi wenye kero au malalamiko kuyafikisha ofisini kwao ili hatua ziweze kuchukuliwa badala ya kunung’unika bila kuchukua hatua.