Back to top

Maombolezo siku tatu kwa waliokufa na Corona Brazil

10 May 2020
Share

Bunge la Brazil limetangaza siku tatu za maombolezo ya taifa, kuwakumbuka watu waliofariki dunia kutokana na janga la virusi vya Corona.

Kwenye mji mkuu Brasilia, bendera ya taifa iliyopo mbele ya majengo ya bunge ilipepea nusu mlingoti kuwaenzi wa athirika wa ugonjwa wa COVID-19.

Idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa huo nchini Brazil  ni zaidi ya Elfu-Kumi na kuifanya nchi hiyo Amerika ya Kusini kuwa ya sita duniani kwa idadi kubwa ya vifo na maambukizi zaidi ya Laki-Moja na Elfu- 48.

Magavana wa baadhi ya majimbo ya taifa hilo wametangaza vizuizi vikali dhidi ya shughuli za umma, serikali ya Rais Jair Bolsonaro inapinga marufuku zilizowekwa na kutoa wito wa kurejea kwa maisha ya kawaida.