Back to top

Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa Sabasaba yafunguliwa Dar.

02 July 2019
Share

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema serikali inapitia upya taasisi zake zote ili kuangalia uwepo wa tozo ambazo bado zimebaki na zinazotozwa katika taasisi zake na itahakisha inaziondoa ili kuweka mazingira mepesi ya biashara yasiyokuwa na urasimu hapa nchini.

Mhe.Samia ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Inocent Bashungwa amesema watahakikisha biashara nchini inakuwa.

Katika maonesho hayo pia Makamu wa Rais alikabibidhi zawadi kwa washindi ambao walifanya vizuri katika maonesho hayo huku pia baadhi ya washiriki wakihimiza kutumia vyema fursa ya Mkutano wa SADIC unaotarajiwa kufanyika Tanzania mwezi ujao.