Back to top

Marekani kuiwekea vikwazo ICC ni kukwamisha utekelezaji wa haki.

04 July 2020
Share

THE HAGUE

____________

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai iliyoko The Hague nchini Uholanzi, Fatou Bensouda amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya taasisi hiyo ya kimataifa vinasikitisha na ni ulipizaji kisasi dhidi ya mahakama hiyo.

Amesema kitendo cha Marekani cha kuiwekea vikwazo mahakama hiyo kimechukuliwa kwa shabaha ya kukwamisha mchakato wa kutekeleza haki na uadilifu.

Mwendesha Mashtaka Mkuu huyo wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai amesema vikwazo hivyo vinafaa kuwekewa magaidi na wanaofanya magendo ya dawa za kulevya na siyo mawakili, wendesha mashtaka au taasisi ya kimataifa.

Majuma kadhaa yaliyopita Rais Donald Trump aliwawekea vikwazo vya kuingia nchini humo wafanyakazi wa mahakama hiyo waliochunguza uhalifu wa kivita uliofanywa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.