Back to top

Marufuku kwa usafiri wa umma Uganda kuendelea kwa siku 14.

04 May 2020
Share

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kwamba marufuku kwa usafiri wa umma,kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja na nusu asubuhi itaendelea kwa siku 14.

Shule za msingi,upili,shule na vyuo vya masomo ya juu zitaendelea kufungwa kwa mda usiojulikana.

Raia wote nchini humo watakaotoka nje ya maboma zao watahitajika kuvalia barakoa.

Endapo mgonjwa wa Corona atathibitishwa sehemu yoyote ya Uganda,eneo zima litawekwa kwenye karantini kwa siku 14.

Raia yeyote anayehisi dalili za homa ya COVID19 nchini humo ametakiwa kupiga simu ya dharura kwa wizara ya afya na sio kwenda hospitalini.wataalamu wa afya watamfikia, kupima sampuli na endapo atapatikana kuathirika atatengwa hospitali,waliotangamana naye wakiwekwa karantini.

Shughuli za ukulima na uzalishaji katika viwanda zitaendelea kawaida,waajiri wakiruhusiwa kuwapa usafiri wa mabasi wafanyakazi wake.

Wafanyakazi wa makampuni wasio na mbinu ya usafiri watatumbia baiskeli au kwenda kwa mguu.

Maduka ya mikahawa yatafunguliwa yakitakiwa kuuza chakula bila mikusanyiko yoyote,kumaanisha mteja atatakiwa kununua chakula na kutoweka.

Maduka ya kuuza bidhaa  za jumla yatafunguliwa wauzaji  wakitakiwa kuzingatia umbali wa kati ya mita 2 na mteja,wateja wakitakiwa kuwa umbali wa mita 4.

Mipaka na anga ya Uganda itasalia kufungwa kwa mda usiojulikana.