Back to top

Marufuku mtoto wa kike kutumikishwa mgodini

18 October 2019
Share

Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wameanza kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria  wazazi wanaowashinikiza watoto wao wa kike  wafanye vibaya kwenye mitihani ya kitaifa kwa lengo la kuwapeleka  kufanya kazi katika machimbo ya  migodi ya dhahabu hali inayopelekea watoto wa kike  kubeba mimba katika umri mdogo.


Akizungumza na wazazi,walimu na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Geita,kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Geita Ritte Adolf anasema wamelazimika kuendesha zoezi hilo ambalo linajumuisha pia watendaji wa kata na vijiji ili kuwanusuru watoto wa kike
 
Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Geita Prisca Rupia anasema mbali na ongezeko la mimba za utotoni pia ni hatari kwa mtoto wa kike kufanya kazi hatarishi kwenye machimbo ya migodi.