Back to top

Marufuku taasisi za umma kutumia maziwa ya unga maofisini.

28 May 2020
Share

Wakati watanzania wakiungana kuadhimisha wiki ya maziwa kitaifa mkoani Dodoma Wizara ya mifugo na uvuvi imepiga marufuku kwa taasisi za umma kutumia maziwa ya unga maofisini na badala yake waanze kutumia maziwa ya ng’ombe yanayozalishwa nchini kama moja ya njia za kukuza viwanda vya ndani.

Hayo yamesemwa na  Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Mh Abdalah Ulega jijini Dodoma wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa ambapo amesema kwa sasa kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka nchini Tanzania ni wastani wa lita 47 pekee kiwango ambacho ni kidogo kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya maziwa Dk.Sophia Mlote amesema tasnia ya maziwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kodi mbalimbali zinazoongeza gharama za uzalishaji.

Akizungumza kwa Niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi amesema wamejipanga katika kuhakikisha wanawekeza kwa wafugaji wa ndani ili waweze kuzalisha kwa wingi na kuongeza pato la nchi.