Back to top

Marufuku wamiliki wa shule binafsi kutoza wazazi fedha za vifaa kinga

28 May 2020
Share

Serikali imepiga marufuku maelekezo yaliyoanza kutolewa na baadhi ya wamiliki wa shule za binafsi ya kuwataka wazazi wenye wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanalipa shilingi laki 7 kabla ya kuripoti shuleni kama gharama za kununulia barakoa, sabuni, ndoo na vitakasa mikono kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kujikinga na corona.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya rais TAMISEMI Mh. Mwita Waitara ametangaza marufuku hiyo jijini Mwanza baada ya kukagua ukarabati wa majengo ya shule kongwe ya sekondari Pamba na kuona maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi 227 wa kidato cha sita katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Fatuma Mashaka pamoja na Afisa Mtendaji wa kata ya Pamba Jonas Mugisha wamepongeza uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli wa kufungua shule na vyuo, huku mafundi wanaoendelea na ukarabati wa majengo hayo wakiezelezea hatua waliyofikia.