Back to top

Marufuku wanafunzi kwenda na 'spirit' shuleni.

28 May 2020
Share

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amepiga marufuku matumizi ya spiriti kama vitakasa mikono kwa shule na vyuo vyote vitakavyofunguliwa kwa kuwa ni hatari.

Aidha Waziri ndalichako amesema kwa vyuo na shule zote zitakazo funguliwa Juni mosi mwaka huu zihakikishe vinaweka vifaa kinga ikiwamo ndoo na maji na sabuni.

Waziri Ndalichako pia amezitahadharisha Taasisi za elimu ikiwamo shule na vyuo ambavyo vimekuwa vikitoa matamko mbalimbali kwa wanafunzi wakati huu vyuo vinafunguliwa kwa kuzitaka taasisi hizo kufuata miongozo iliyotolewa na  wizara ya afya pekee na sio kila taasisi kutengeneza miongozo yake.