Back to top

Masasi waagizwa kujenga majengo mengine shule ya Msingi Mpohora.

24 February 2021
Share

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde ameiagiza Halmashauri ya Masasi iliyopo mkoani Mtwara kujenga majengo mengine katika shule ya Msingi Mpohora baada kukuta madarasa mabovu ambayo yanaweza kuwaangukia wanafunzi muda wowote. 


Mh. David Silinde ameyasema hayo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea mazingira wanayosomea wanafunzi shuleni hapo na kuahidi kuingiza fedha kiasi cha milioni 40 ambayo ni nje ya bajeti na kuwaahidi wanafunzi na walimu, kuwa shule hiyo itaingizwa katika bajeti ya kujengewa madarasa mengine mapya.