Back to top

Masele atinga bungeni,kutii wito wa spika Ndugai.

20 May 2019
Share

Makamua wa Rais wa kwanza wa bunge la Afrika na mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele amewasili bungeni tayari kwa kuhojiwa na kamati ya bunge kinga na maadili ya bunge kama ilivyoelekezwa na Spika wa bunge Mhe Job Ndugai wiki iliyopita.

Baada ya Mh Masele kuingia bungeni spika wa bunge mhe Ndugai alitangaza kuwa kamati ya maadili itoke na ikutane tayari kwa kikao hicho.

Mh Masele amekaririwa na vyombo mbalimbali ya habari vikiwemo vya nje akiahidi kufika leo bungeni kuja kuhojiwa na kuambiwa makosa yake kwani hajui kosa lake halisi.