Back to top

Mashine tano zafungwa JNIA kukabiliana na wagonjwa wa CORONA.

31 January 2020
Share


Kitengo cha Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza, kilichopo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kimejipanga kukabiliana na wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya homa ya Corona, vilivyoanzia nchini China.

Mdhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza wa wa kiwanja hicho Dakta George Ndaki amesema wizara hiyo imekabiliana na ugonjwa huo na tayari imefunga mashine tano zinazotumia kompyuta zinazopima joto la mwili la abiria bila kujitambua na mashine sita za mkononi, ambazo abiria anapimwa endapo ataonekana kuwa na joto kali zaidi.

Amesema mashine moja imefungwa kwenye Jengo la Watu Mashuhuri, nyingine imefungwa jengo la pili la abiria na nyingine tatu zipo jengo la Tatu la abiria.

Amesema hadi sasa hakuna abiria aliyebainika kuwa na ugonjwa huu, lakini hiyo inaendelea kwani kwanja hicho cha ndege ni moja ya njia kuu au lango Kuu la abiria kuingia na kutoka nchini.