Back to top

Mashine ya kuchemshia korosho yalipuka yaua mmoja yajeruhi wawili.

12 April 2019
Share

Mtu mmoja amefariki na wawili kujeruhiwa baada ya mashine ya kuchemshia korosho kulipuka wakati walipokuwa kwenye mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho yanayotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Lindi.

Akizungumza na ITV/Radioone Katibu wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine, Bwana.Boniface Lymo, amesema leo majira ya saa nne na nusu asubuhi walipokea majeruhi wawili na mtu mmoja akiwa amefariki aliyejulikana kwa jina la Sada Juma (28).

Amesema marehemu alipata majeraha makubwa kwenye eneo la shingo na koo na jeraha hilo limetokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali kilichosababisha kuvuja damu nyingi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Pudencian Protas, amethibitisha kutokea kwa tuko hilo.