Back to top

MAZUNGUMZO KUMALIZA VITA KATI YA JESHI LA ETHIOPIA NA TPLF

26 October 2022
Share

Mazungumzo rasmi ya kwanza ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya miaka miwili kati ya jeshi la Ethiopia na kundi la wapiganaji wa TPLF yameanza rasmi nchi afrika kusini.

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na Umoja wa Afrika, yameanza wakati wanajeshi wa serikali ya Ethiopia, wakipiga hatua katika uwanja wa mapambano, kwa kuikamata miji mikubwa kadhaa katika jimbo la Tigray wiki iliyopita.

Mazungumzo hayo yanachukuliwa kama fursa ya kuumaliza mzozo huo uliosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Mzozo huo pia umewaacha maelfu ya watu katika ukingo wa njaa katika taifa hilo ambalo ni la pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Oparesheni ya serikali, iliyofanywa kwa pamoja na washirika wake kutoka Eritrea imeibua wasiwasi wa kutokea madhara kwa raia.