Back to top

Mbunge wa Rorya aagiza baba mdogo wake kukamatwa na Polisi

15 October 2018
Share

Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya katika wilaya ya kipolisi ya Rorya limemkamata baba mdogo wa mbunge wa jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo kwa maagizo ya mbunge huyo baada ya kutajwa katika mkutano wa hadhara kujihusisha na tuhuma za wizi wa mifugo,ikiwa ni sehemu ya kampeni inayofanywa na vyombo vya dola wilayani humo ya kupambana na wimbi kubwa la wizi wa mifugo ambalo limeibuka katika siku za hivi karibuni wilayani humo.
 
Hatua hiyo imechukuliwa na mbunge huyo wa jimbo la Rorya Mhe. Lameck Airo katika mkutano wa hadhara katika kijiji Koryo wilayani Rorya kufuatia wananchi wa kijiji hicho kumtaja mzee huyo katika mkutano wa hadhara kuwa amekuwa akiiba Ng'ombe na kuuza katika minada ya ndani na nje ya wilaya hiyo.
 
Akizungumza katika mikutano hiyo ya kupambana na wizi wa mifugo wilayani Rorya,mkuu wa polisi wa wilaya ya Rorya Ramadhan Sarige,amewapongeza ushirikiano ambao umeanza kutolewa na wananchi kwa vyombo vya dola katika kukabiliana na vitendo hivyo vya wizi wa mifugo.