Back to top

Mbwa wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa kichaa waua na kujeruhi Gairo.

16 April 2021
Share

Mbwa wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa wamekuwa tishio katika wilaya ya Gairo mkoani Morogoro baada kumg’ata mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na kufariki kisha kujeruhi watu wengine sita kwa nyakati tofauti hali iliyo lilazimu baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kutoa siku  10 kwa wataalamu wa afya ya wanyama kudhibiti wanyama hao kabla hawajasababisha madhara makubwa.
.
Kufuatia hali hiyo Afisa mifugo na uvuvi wa wilaya ya Gairo  Dr.Godbless Luhunga  amesema  watapunguza  idadi ya kuzaliana kwa mbwa hao.