Back to top

Mechi za UEFA Champions League na UEFA Europa League zaahirishwa.

13 March 2020
Share

Shirikisho la soka barani ulaya (UEFA) limetangaza kuahirishwa kwa mechi zote za UEFA  Champions League na UEFA Europa League kuanzia wiki ijayo hadi ifikapo April 3 kufuatia tishio la virusi vya Corona.

kuahirishwa huko pia kunahusisha ligi ya UEFA ya vijana, na katika kuahirisha huko pia kumesababisha hata droo za robo fainali ya UEFA Champions League na UEFA Europa League zilizokuwa zimepangwa kufanyika tarehe 20 mwezi Machi nayo kuahirishwa.