Back to top

Merkel azitaka nchi za Umoja wa Ulaya kuonesha mshikamano.

09 July 2020
Share

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kuonesha mshikamano na kuondoa migawanyiko iliyopo ili kuidhinisha mpango wa kuuokoa uchumi wa Ulaya ulioathiriwa na janga la virusi vya corona.

Merkel amesema hayo alipokutana na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel na Spika wa Bunge la Ulaya, David Sassoli kwa ajili ya kuuandaa mkutano wa viongozi wa nchi 27 za umoja huo utakaofanyika wiki ijayo.

Merkel amesema Ulaya inahitaji mshikamano mkubwa na kwamba kila mmoja yuko tayari na hasa Ujerumani ili kuondokana na janga la COVID-19 pamoja na kukabiliana na athari zake.