Back to top

Mfumo wa malipo kupitia benki washindwa kuwasaidia wakulima wa Pamba.

07 May 2021
Share

Serikali imesema kupitia msimu wa manunuzi wa zao la pamba kwa mwaka 2020/2021 iliratibu  kwa majaribio mfumo wa kulipa wakulima wa zao hilo kupitia njia za kibenki na simu za mikononi  mfumo ulioonekana kutosaidia wakulima hao.

Naibu waziri wa kilimo Mh.Hussein Bashe amesema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu wakati akijibu swali la Mh.Ester Lukago Midimu - Viti Maalum aliyetaka kufahamu mkakati wa serikali wa kuwalipa wakulima wa zao la pamba katika msimu wa manunuzi unaotarajiwa kuanza Mei hadi Julai mwaka huu.

Aidha, Mh.Hussein Bashe amesema kutokana na mfumo wa awali uliotumika katika kuwalipa wakulima kuonekana kuwa na ubadhirifu wa fedha sasa serikali itaruhusu wakulima kulipwa fedha zao taslimu hususani kwa maeneo ambayo hakuna mabenki.