Back to top

Mgogoro wa ardhi waibuka baada ya mwenyekiti kuokota dhahabu.

09 January 2019
Share

Maelfu ya wananchi wamefurika kwenye shamba la Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugege mzee Clement Busiga aliyeokota jiwe la madini ya dhahabu shambani kwake wakati akichimba mashimo ya kupanda migomba ya ndizi hali iliyosababisha mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha lwantaba na kijiji cha Makurugusi wilaya ya Chato mkoa wa Geita wakigombea mipaka.

ITV imeshuhudia maelfu ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu wakiwa wamevamia shamba lenye mazao mbalimbali ya chakula likihalibiwa ikiwemo mihogo na mahindi iking’olewa ili kupisha eneo la kuchimbwa mashimo kwa lengo la kutafuta madini ya dhahabu chini ya ardhi huku magari ya mizigo na pikipiki zikitumika kusafilisha madini hayo.

Baada ya mgogoro huo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Chato ikawasili kwenye eneo la tukio na kuweka utaratibu unaotakiwa ikiwemo kupanga safu ya uongozi wa mgodi huo.