Back to top

Mhe.Rais Samia awatakia Waislamu Mfungo mwema wa Mwezi wa Ramadhani.

13 April 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewatakia Waislamu wote mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, huku akisisitiza kuwa katika kipindi hicho cha toba wasisahau kuiombea nchi Amani, Upendo, Mshikamano na Utulivu.

Mhe.Rais Samia Suluhu katika ukurasa wake wa Twitter ameandika ujumbe huo.

"Nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tukiwa katika kipindi hiki cha toba tusisahau kuiombea nchi yetu amani, upendo, mshikamano na utulivu ili kujenga mazingira bora zaidi kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Ramadhan Kareem wa Swaum Maqbul"-Mhe.Rais Samia Suluhu Hassani.

Hata hivyo Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi jana alimsema kuwa Waislamu wataanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Aprili 14, 2021, baada ya Aprili 12 mwezi kutoonekana.

Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi.

Wakati Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi akitangaza Jana kutoonekana kwa mwezi, Baadhi ya Waislam nchini ikiwemo "Answar Sunna" wameungana na mataifa mengine ulimwenguni ambayo yameeleza kuona mwezi na kuanza kufunga leo Aprili 13, 2021.