Back to top

Miezi 2 yatolewa bodi ya maji ifikishe maji uwanja wa ndege Chato.

12 June 2020
Share

CHATO MKOANI GEITA.

Serikali imeipa miezi miwili Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ifikishe maji katika uwanja wa ndege wa Chato kutoka kwenye mradi mkubwa wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni nne, ili kuhakikisha huduma za maji zinapatikana muda wote katika uwanja huo.

Akikagua ujenzi wa miradi ya maji na uwanja wa ndege Chato Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema serikali kupitia wataalam wa ndani wametekeleza miradi mikubwa mitatu ya maji ambayo itamaliza tatizo la maji kwa mkoa wa Geita na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kagera.

Wakazi wa wilaya ya Chato wameipongeza serkali kwa ujenzi wa miradi ya maji na kuiomba ichimbe visima vingine katika maeneo ambayo visima vilivyopo havitoi maji.