Back to top

Mifuko ya sukari zaidi ya 148 iliyokamatwa Tanga yataifishwa.

11 February 2019
Share

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Pangani kwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) mkoa wa Tanga wamekamata na kuitaifisha shehena ya mifuko ya sukari zaidi ya 148 iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria ikitokea india kupitia kisiwani Zanzibar tayari kusafirishwa kwenda nchi jirani ya Kenya.

Shehena hiyo imekamatwa katika bandari bubu ya Kipumbwi iliyopo wilayani Pangani wakati ikiwa katika harakati za kusafirishwa kwenda makao makuu ya wilaya kisha jijini Tanga hadi nchi jirani ya Kenya na sukari hiyo imebaini kuwa ni ya kutoka nchini India.