Back to top

Miili ya Wafanyakazi 5 wa Azam Media yaagwa Tabata Dar Es Salaam.

09 July 2019
Share

Viongozi mbalimbali , watendaji wakuu wa vyombo vya habari na wanahabari wameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar Es Salaam katika zoezi la kuagwa kwa miili ya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited waliofariki katika ajali baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kizonzo, katikati ya Igunga mkoa wa Tabora na Shelui mkoa wa Singida.

Zoezi hilo limefanyika Makao Makuu ya Ofisi za Azam Tabata Jijini Dar Es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko katika maeneo mbalimbali ambayo ndugu wameyachagua.

Ajali iliyosababisha vifo vya wafanyakazi hao wa Azam Media ilItokea jana majira ya saa 2:30 asubuhi katika eneo la Kizonzo, katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo basi aina ya Coaster iililowabeba wafanyakazi hao likielekea Mwanza liligongana uso kwa uso na Lori la mizigo lililokuwa linakwenda Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao Azam Media Limited walikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kwa ajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.