Back to top

Mikokoteni kusajiliwa Zambia kudhibiti wizi.

27 July 2020
Share

Zambia imepanga kusajili mikokoteni yote ambayo inayotumika kwa matumizi ya kibiashara kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la  vitendo vya wizi hivyo wasukuma mikokoteni hao wameshauriwa kusajili mikokoteni yao katika shirikisho la wasukuma mikokoteni nchini humo.

Wafanyabiashara wengi wa nchi hiyo hupenda kutumia wasukuma mikokoteni kusafirisha bidhaa zao kutokana na unafuu wa gharama za ubebaji.

Hayo yamebainishwa na Meya wa Lusaka bwana Miles Sampa ambapo amesema kumekuwa na ongezeko la malalamiko ya uhalifu kutoka kwa wafanyabiashara wanaotumia sana huduma hiyo hivyo wameamua ameamua kuanzisha malipo ya kodi ya mikokoteni hiyo.