Back to top

Milioni 681 zatengwa kukarabati na kujenga minada ya mifugo nchini.

02 August 2020
Share

Serikali katika bajeti ya mwaka 2020/ 2021 imetenga Shilingi Milioni 681 kwa ajili ya kukarabati na kujenga minada ya mifugo nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt.Felix Nandonde alipofanya ziara ya kukagua ukarabati unaoendelea kufanywa katika Mnada wa Ipuli Mkoani Tabora.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo alisema kuwa Wizara imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuboresha minada hiyo ili kuongeza tija katika biashara hiyo na kukuza mapato ya serikali.

Ameongeza kuwa ujenzi wa mnada wa kimkakati mpakani mwa Tanzania na Burundi utasaidia kutatua tatizo la muda mrefu la eneo la Tanzania kugeuzwa eneo la kuchunguia mifugo na utafanya Tanzania kupata mapato kupitia mnada huo.