Back to top

Minada ya Korosho na ufuta kufanyika kwa njia ya Kieletroniki.

12 April 2021
Share

Katika kuongeza thamani ya zao la Korosho na ufuta hapa nchini serikali imesema katika msimu ujao wa uuzaji wa mazao hayo minada yake itafanyika kwa njia ya kieletroniki ambayo itaaanza mapema kabla ya minada kuanza.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti Mhe.Twaha Mpembenwe aliyetaka kujua ni njia zipi zinatumiwa ma serikali katika kudhibiti mporomoko wa bei ya korosho na ufuta katika soko la dunia na kusababisha wakulima kupata hasara kwa kupata bei ndogo wanapouza korosho zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vigezo vya ubora wa korosho hizo.

Mhe.Bashe amesema mpango huo pia unakwenda sawia na kutoa elimu kwa wakulima wa korosho ili kuzingatia ubora wa korosho zisizokuwa na unyevuunyevu ambazo nyingi zimekuwa zikirudishwa kwa wakulima katika minada inayofanyika kwa sada na kuzua malalamiko mengi kwa wakulima kutokana na korosho hiyo kuharibika kabla haijafika sokoni.

Kutokana na hatua ya kuanzishwa kwa minada ya kieletroniki mpango huo utasaidia pia kupatikana kwa masoko mengi yakiwemo ya kimataifa.