Back to top

Minada ya Korosho yatakiwa kufunguliwa ili korosho za wakulima ziuzwe.

18 September 2021
Share

Naibu Katibu Mkuu wa CCM TaifaChristine Mndeme amesema minada ya Korosho katika msimu wa mwaka huu wa 20/21 hauna budi kufunguliwa  kwa wakati ili korosho za wakulima ziweze kuuzwa kwenye mfumo sahihi na kunufaika na zao hilo.
.
Mndeme ametoa kauli hiyo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Newala wakati akikagua ujenzi wa miradi ya maendeleo  yakiwemo madarasa, vyoo na ujenzi wa hospitali ya wilaya Newala.

Amesema ucheleweshaji wa ufunguzi wa minada umekuwa ukipelekea wakulima kulanguliwa korosho kutokana na uhitaji wa fedha hivyo ametaka viongozi wa mkoa kuhakikisha minada hiyo inafunguliwa kwa wakati.
.
Hata hivyo amesema serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira mazuri kwa wakulima wa korosho ikiwa ni pamoja na kutoa pembejeo bure, sambamba na kuondoa baadhi ya tozo kwenye zao hilo ili mkulima aweze kunufaika.
.
Minada ya korosho inatarajiwa kufunguliwa tarehe moja ya mwezi wa kumi mwaka 2021.