Back to top

Mitambo 5 ya kupakulia shehena ya mizigo imewasili bandari ya Tanga

08 December 2018
Share

Mitambo mitano ya kisasa ya kupakulia shehena ya mizigo kati ya mitambo 20 iliyopangwa kununuliwa imewasili katika bandari ya Tanga ili kurahisisha upakuaji wa mizigo katika bandari hiyo.

Ununuzi wa mitambo hiyo ni miongoni mwa mafanikio ya miaka mitatatu ya serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Magufuli ikiwa ni mwelekeo wa mipango ya serikali hiyo katika kuhakikisha bandari nchini znapata watumiaji wengi na kuinua uchumi wa taifa.

Mkuu wa bandari ya Tanga Bw.Percival Salama anasema wanaifanyia marekebisho mbalimbali bandari hiyo ili kuruhusu meli kubwa kuweza kutia nanga na kuendana na mradi mkubwa mafuta ghafi kutoka Oima Uganda hadi Chongoleani Tanga.

Bw.Salama anasema kuwa vifaa vingine vilivyowasili ni pamoja na boti ya kisasa ya doria,magari ya zimamoto na Scaner ya kisasa ya ukaguzi wa mizigo na kwamba katika miaka mitatu ya serikali ya Rais Dkt. Magufuli bandari hiyo imeomeondoa malalamiko mbalimbali ya ucheleweshaji wa mizigo na kufanikiwa kuwarejesha wateja wake wa ndani na nje ya nchi.