Back to top

Mkandarasi wa mradi wa umeme Kinyerezi One afilisika, mradi wakwama.

25 February 2020
Share

Kampuni ya Jacobsen elektro ya  nchini Norway iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme Kinyerezi One Extension imeshindwa kuendelea na ujenzi baada ya  kufilisika jambo  linalosababisha mradi huo wa Megawatt 185 kutokamilika kwa wakati.

Hayo yamebainika jijini Dar es salaam wakati Bodi ya wakurugenzi ya shirika la ugavi wa umeme (TANESCO) ilipokuwa ikitembelea mradi wa kufua umeme kwa gesi asilia uliopo Kinyerezi ambapo Mwenyekiti wa bodi Dk Alexander Kyaruzi amesema kutokana na hatua hiyo kwa sasa imeundwa tume maalum ambayo itamuhusisha mwanasheria mkuu wa serikali ili kushughulikia swala hilo pamoja na kumpata mkandarasi mpya.

\
Mkandarasi huyo ambaye alianza kazi mwezi wa nane mwaka 2016 na ilikuwa amalize mwezi wa sita 2018 ambapo serikali ya Tanzania imemlipa fedha zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 128 huku gharama ya mradi ikiwa ni dola milioni 188.