Back to top

Mkataba bubu wa zaidi ya Trilioni 1 wamg'oa Lugola na Andengenye.

23 January 2020
Share

Rais Dkt.John Pombe Magufuli amemwondoa kwenye nafasi yake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kwa kutoridhishwa na utendaji wao.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi nyumba za Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amempongeza Katibu Mkuu wa   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu kwa kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake kutoka na ufisadi uliofanywa na kikosi cha zimamoto kilichopo chini ya wizara hiyo.

Rais Magufuli amesema haridhishwi na utendaji wa kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana kuandaliwa mkataba wa mradi wa ajabu wa gharama ya Euro mia nne na nane ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni moja katika mazingira yenye utata, bila kufuata  taratibu na kampuni moja ya nchini Romania.

Aidha, amewataka wasaidizi wa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tthobias Andengenye waliohusika na kuandaa mkataba huo nao wajitathimini huku akiwapongeza Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuona umuhimuu wa kuwajibika.

Akiongea baada ya tamko hilo, Mhe.Kangi Lugola amekubaliana na uamuzi wa Rais.

MAGUFULI AMTUMBUA ANDENGENYE NA LUGOLA, VIDEO IPO HAPA