Back to top

Mkazi wa Geita atupwa jela miaka 7 kwa kumuua kwa kumyonga mtoto wake

19 September 2019
Share

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imemuhuku kifungo cha miaka saba gerezani, Shija Hamisi mkazi wa Kijiji cha Runzewe Kata ya Unyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kwa kosa la kumuua kwa kumnyonga shingo mtoto wake mchanga mwenye umri wa siku kumi na nne kisha kumtelekeza.

Alichukua hatua hiyo kutokana na ugovi wa mapenzi akimtuhumu mkewe kubeba ujuzito nje ya ndoa.

Akisoma hukumu hiyo katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Geita, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mheshimiwa Upendo Madehe amesema, Februari 4, 2014 majira ya saa moja jioni Shija Hamisi mwenye umri wa miaka ishirini na sita alimuua kwa kumnyonga shingo mtoto wake wakati mke wake akiwa nje ya nyumba.

Jaji upendo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 195 na kifungu cha 198 hivyo mtuhumiwa amekutwa na hatia na anapewa adhabu ya kwenda jela miaka saba.