Back to top

Mkulima wa Kahawa kupata ahueni bei kutoka shambani hadi sokoni.

16 April 2021
Share

Serikali imesisitiza kuweka mazingira mazuri ya kuimarisha bei ya zao la Kahawa kuanzia shambani hadi sokoni na kupiga marufuku wafanyabiashara wanaonunua kahawa ikiwa shambani hatua hiyo ni sawa na kumnyonya mkulima inapofika wakati wa msimu wa mauzo ya zao hilo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe wakati akijibu swali la Mhe.Anatropia Theonest Mbunge wa viti maalumu CHADEMA aliyetaka kujua serikali ina mpango gani kubadilisha mfumo wa ununuzi wa kahawa kwa wakulima kutoka shambani na kuwanyonya wakulima.

Naibu wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe.

Mhe.Bashe amesema kiwango cha uzalishaji wa zao la Kahawa imeendelea kuongezeka kutoka mwaka 2016 tani elfu 47 mpaka kufukia tani elfu 59 mwaka 2019/2021 na kuonesha mwenendo mzuri wa kuimarika kwa zao hilo kwa kila mwaka.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo ameongeza kuwa katika kuwasaidia zaidi wakulima serikali imejipanga kuimarishwa zaidi vyama vya ushirika kwa kusaidia wakulima kuepukana na wafanyabiashara wanyonyaji wanaonunua kahawa ikiwa shambani kwa sasa kwa baadhi ya wakulima.