Back to top

Mkurugenzi wa UDART na wenzake watatu wasomewa mashtaka 19.

11 February 2019
Share

Mkurugenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi UDART,Bwana Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashitaka 19 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam ikiwemo shtaka la utakatishaji fedha wa Shilingi Milioni 603 pamoja na kuisababishia hasara mradi wa UDART ya Shilingi Bilioni 2.41 .

Mbali ya Bwana Kisena, washitakiwa wengine ni Kulwa Kisena, Charles Newe na Cheni Shi ambaye ni  raia wa China .

washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Bwana George Barasa na Moza Kasubi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Bwana Thomas Simba.