Back to top

Mkutano wa 13 wa Bunge la 11 kuanza Novemba 06,2018 Dodoma.

05 November 2018
Share

Mkutano wa  13 wa bunge la 11 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaanza kesho mkoani Dodoma huku baadhi ya mambo yatakayojadiliwa na bunge hilo ni mpango wa  taifa kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambao unaakisi bajeti ya serikali kwa mwaka huo wa fedha na pia maazimio matatu kujadiliwa na kisha kupitishwa na bunge hilo.

Spika wa bunge hilo Mhe.Job Ndugai amesema kwenye mkutano huo wabunge wateule wanne wa majimbo ya Korogwe vijijini, Ukonga ,Monduli na Liwale kula viapo na kuwa wabunge kamili na wabunge wengine wanne waliotangazwa mwishoni mwa wiki iliyomalizika wataapishwa bunge lijalo.

Spika Ndugai amesema mbali ya hayo kutakuwa na miswada minne ikihusu sheria mbalimbali ambayo itasomwa kwa mara ya kwanza na muswada wa sheria ya mabadiliko ya huduma ndogo za fedha ambao utasomwa kwa hatua zote kusubiri saini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili uwe sheria.

Baadhi ya wabunge waliozungumza na ITV wamesema mkutano huo ni muhimu kwa taifa kwani utawawezesha kuvifahamu vipaumbele vya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 na wao kutumia fursa hiyo kuviboresha huku wananchi wa kawaida wakisema wanatumai  changamoto ambazo zinawakabili watanzania katika nyanja mbalimbali zitatuliwa.