Back to top

Mkuu wa JKT aomba kupatiwa baadhi ya samani za Makonda.

10 October 2018
Share

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT nchini Meja Jenerali Martin Busungu ameiomba serikali kulipatia jeshi hilo sehemu ya samani za ndani zilizopo kwenye makontena yaliyoingizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ambazo kwasasa zinashikiliwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA.

Meja Jenerali Martin Busungu ametoa ombi hilo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dokta Hussen  Mwinyi akimuomba kuwasiliana na Waziri wa Fedha ili kuona uwezekano wa kupata samani hizo kwaajili ya jengo la utawala katika shule ya sekondari Kawawa inayomilikiwa na Jeshi hilo kikosi cha 841 Mafinga.