Back to top

Mkuu wa kitengo cha fedha TRC asimamishwa kwa kutowalipa wafanyakazi.

15 February 2020
Share

Waziri wa Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano  Mhandisi Isack Kamwelwe ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa kitengo cha fedha wa Shirika la Reli nchini (TRC) Emmanuel Balele kutokana na kushindwa kuwalipa mshahara kwa muda mrefu, wafanyakazi wa reli wanaohusika kulinda na kukarabati  kipande cha reli kilichozolewa na maji, maarufu kama pigilia, eneo la Msagala mpaka Gulwe wilayani Kilosa Mkoani Morogoro

Waziri Kamwelwe amefikia uamuzi huo baada ya kutembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko yaliyosomba kipande cha reli ya kati inayotoka mikoa ya kanda ya ziwa hadi Dar es salaam, kipande cha zaidi ya kilometa 120 .