Back to top

Mkuu wa mkoa wa Lindi amewataka watumishi wa umma kufuatilia maelekezo

14 April 2019
Share

Mkuu wa mkoa wa Lindi,Bw.Godfrey Zambi, amewataka watumishi wa umma kufuatilia maelekezo ya viongozi wa kitaifa wanapokuwa kwenye ziara zao kwa sababu mara nyingi ndiko wanakotoa maelekezo ya jumla.

Mkuu wa mkoa wa Lindi ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi pamoja na wataalam wa sekta ya afya huku akiwataka watumishi hao kutekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi wao wa wilaya ama mkoa.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Lindi, Bi.Rehema Madenge, amewashauri wananchi pamoja na viongozi katika wilaya zao kuendelea kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao hasa kipindi cha mvua.