Back to top

Mlipuko waleta maafa makubwa Lebanon, hali ya dharura yatangazwa.

05 August 2020
Share

Rais wa Lebanon Michel Aoun ameitisha kikao cha dharura na baraza lake la mawaziri leo Jumatano na kutangaza wiki mbili za hali ya dharura nchini humo kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea mjini Beirut uliouwa zaidi ya watu 70 na kujeruhi 4000.

Lebanon imeanza siku tatu za maombolezo kuanzia leo Jumatatu.

Zoezi la uokoaji linaendelea nchini Lebanon kwa kufukua vifusi ,idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Ripoti mbalimbali zinasema kuwa mlipuko mkubwa umetokea kwenye eneo la bandari la mji huo, huku kukiwa hakuna ripoti za kutokea kwa mlipuko wa pili. Mamlaka zinahofu kutokea kwa madhara makubwa.

Waziri mkuu wa Lebanon Hassan Diab amesema kwa yeyote atakaebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine na mlipuko huo uliosababisha vifo na majeruhi nchini humo kuwajibishwa ipasavyo.
 

Mpaka sasa kilichosababisha mlipuko huo haujajulikana,kikosi kazi maalum kinaendelea kutafuta chanzo na kuahidi kumuwajibisha yeyote atakaehusika.