Back to top

Mradi wa kuwafunga tembo vifaa maalum vya kisasa wakamilika.

12 September 2018
Share

Shirika la Kimataifa la Uhifadhi  wa Mazingira la WWF, kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori Tanzania TAWIRI limekamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa  kuwafunga tembo vifaa maalum vya kisasa vitakavyotumika kufuatilia nyendo zao kama njia ya kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori hao nchini Tanzania.


Mradi huo ambao umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 300 fedha zilizotolewa na Shirika la WWF la nchini Sweden umetekelezwa katika ikolojoa ya pori la Akiba la Selou umeshirikisha wadau wengine wa uhifadhi ikiwemo Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA na Mamlaka ya wanyamapori Tanzania.