Back to top

Msako wa magari mabovu waendelea Mkoani Shinyanga

10 July 2018
Share

Jeshi la la polisi mkoani Shinyanga limeendelea kusaka na kuyakamata magari mabovu na kuwachukulia hatua madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani kwa lengo la kutekeleza agizo la serikali la kutokomeza ajali zinazosababishwa na uzembe.

Akizungumza na kuonyesha baadhi ya magari  yaliyokamatwa na kuzuiliwa katika kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Shinyanga mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha mkoa huo Bw. Anthony Gwandu amesema katika msako ambao inaendelea wilayani Shinyanga magari zaidi ya 20 mabovu yamekuwa yakikamatwa kila siku huku mengine yakiwa hayana sifa za kuendelea kutoa huduma kwa kutumia barabara.

Nao baadhi ya madereva wa magari hayo yaliyokamatwa wamesema baadhi ya matajiri wa magari wamekuwa wagumu kutengeneza magari yanapoharibika hali inayosababisha yazidi kuwa mabovu licha ya kupokea fedha za kila siku.

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Shinyanga Bw.Emmanuel Pallangyo amesema msako unaoendekea sio kwa magari ya abiria na ya mizigo lakini utahusika pia na pikipiki, baiskeli na na matela ya kukokotwa na wanyama kwakuwa vyombo hivyo vyote vinatumia barabara na vimekuwa vikisababisha ajali mara kwa mara.