Back to top

Mtoto auawa kwa panga na anayedaiwa kuwa baba wa kambo.

03 January 2020
Share

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu Caren Crispine ameuawa kikatili na baba yake wa kambo aliyetajwa kwa jina la Leonard Kishenya mwenye umri wa miaka 36, mkazi wa kijiji cha Katorerwa wilayani Misenyi mkoani Kagera anayetuhumiwa kumkata kata kwa mapanga na kutenganisha baadhi ya viungo vya mwili wake.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo, kamishina Msaidizi, Revocatus Malimi amesema mtu huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo usiku wa kuamkia jana baada ya kuzuka ugomvi kati yake na mke wake aliyemtaja kwa jina la Domina Andrew mwenye umri wa miaka 30.