Back to top

Mtu mwenye asili ya Ujerumani amekamatwa mkoani Mbeya akiwa na gobole.

13 February 2019
Share

 

Mtu mmoja mwenye asili ya Ujerumani anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya baada ya kukutwa na bunduki aina ya gobole ambalo limetengenezwa kienyeji, huku pia akiwa hana vibali vya kuingia wala kuishi nchini.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamshna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la polisi, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika maeneo ya Makasini, Uyole jijini Mbeya.