Back to top

Mtuhumiwa wa mauaji ya vikongwe kwa mapanga akamatwa Shinyanga

12 October 2018
Share

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limemkamata na kumshikilia mtu mmoja (30) mkazi wa Ushetu wilayani Kahama kwa tuhuma ya kuwaua wanawake vikongwe kwa kuwakata mapanga huku watuhumiwa wengine 57 wanashikiliwa wakituhumiwa kujihusisha na makosa mbalimbali ikiwemo kutumia na kuuza wa dawa za kulevya aina ya bangi na heroine, utapeli ,wizi wa magari na pikipiki na utengenezaji wa pombe haramu ya moshi ambapo mitambo 11 na lita 200 za pombe hiyo ya Moshi zimekamatwa katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga.


Akitoa taarifa ya kukamatwa watuhumiwa hao kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa mtuhumiwa huyo wa mauaji kwa kutumia mapanga Bw.Fikiri Charles amekamatwa majira ya saa10 alfajiri wakati anajiandaa kwenda kutekeleza mauaji ya mama mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama na alipohojiwa amekiri kuwaua wanawake wengine 6 katika maeneo mbalimbalinya mkoa wa Shinyanga na kudai kuwa kazi hiyo ameirithi kutoka kwa baba yake mzazi.